1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiColombia

Colombia yaongoza kwa mauaji ya wanaharakati wa mazingira

13 Septemba 2023

Shirika la Uangalizi lisilo la kiserikali la "Global Witness" limeitaja Colombia kuwa nchi hatari zaidi duniani ambayo inaongoza kwa mauaji ya wanaharakati wa mazingira.

https://p.dw.com/p/4WGVd
Kolumbien Bogot | Demo für und gegen Abtreibungsrecht
Picha: Fernando Vergara/AP/picture alliance

Katika ripoti yake ya kila mwaka, shirika hilo lenye makao yake mjini London, Uingereza limesema mauaji dhidi ya wanaharakati wa mazingira yameongezeka maradufu nchini  Colombia mwaka jana, huku ikitoa orodha ya watetezi 177 wa ardhi na mazingira ambao waliuawa mwaka 2022 kuanzia Ufilipino hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Idadi ya waliouawa imepungua kidogo ukilinganisha na rekodi ya watu 227 waliouawa mwaka 2020, lakini shirika la Global Witness limesema hii haimaanishi kuwa kwa kiasi kikubwa hali imeboreka.

Shirika hilo limesisitiza kuwa kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa za kilimo, mafuta na madini kutazidisha shinikizo kwa mazingira pamoja na wanaharakati wanaohatarisha maisha yao ili kuilinda sayari.