1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Watu kumi wauawa katika kiunga cha mji wa Port-au-Prince

19 Machi 2024

Watu wasiopungua kumi wameuawa kwenye kiunga cha matajiri katika mji mkuu wa Haiti jana Jumatatu, ambapo pia kumeripotiwa uporaji, na wizi wa vifaa vya umeme uliosababisha kukatika kwa umeme.

https://p.dw.com/p/4dsiz
Haiti, Port-au-Prince | Wahaiti wakiwa wamekusanyika na miili ya waliopigwa risasi na kufariki.
Maelfu ya Wahaiti wakiwa wamekusanyika huku wakibeba miili ya watu waliopigwa risasi, wakati vurugu zikiongezeka nchini humoPicha: Ralph Tedy Erol/REUTERS

Wakati hayo yakiendele vurugu zimeripotiwa kusambaa katika maeneo ya matajiri, na magenge yakiimarisha udhibiti wao kwa mji huo.

Shuhuda wa shirika la habari la Reuters aliona miili isiyopungua kumi, ambayo baadhi yake ilikuwa na matundu ya risasi, katika mitaa ya kiunga cha Petion-Ville kwenye kingo za mji wa Port-au-Prince, ambayo baadae iliondolewa na magari ya kusafirisha wagonjwa. Hata hivyo mamlaka hazikuzungumzia mazigira ya vifo hivyo.

Soma pia:Umoja wa Mataaifa waonya juu ya hali mbaya nchini Haiti

Wahaiti pia wameripoti milio ya risasi na uporaji jana asubuhi katika eneo la karibu la Laboule, na baadae mitaa ya Petion-Ville ilitelekezwa. Shirika la umeme la EDH lilisema vituo vyake kadhaa vilishambuliwa, na kwamba kebo, betri na nyaraka viliibwa.