1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Ufaransa kupeleka ndege maalum kuwaondoa raia wake Haiti

Bruce Amani
25 Machi 2024

Ufaransa itapeleka ndege maalum kwa ajili ya kuwaondoa nchini Haiti raia wake walioko hatarini zaidi. Safari za ndege kutoka na kuingia mji mkuu Port-au-Prince zilikatizwa kutokana na vurugu za kisiasa.

https://p.dw.com/p/4e4v3
Kuna makabiliano kati ya polisi na magenge ya uhalifu Port-au-Prince
Magenge ya uhalifu yanaendelea kusababisha machafuko katika mji mkuu Port-au-PrincePicha: Ralph Tedy Erol/REUTERS

Ufaransa itapeleka ndege maalum kwa ajili ya kuwaondoa nchini Haiti raia wake walioko hatarini zaidi. Haya yamesemwa na Wizara ya mambo ya kigeni ya Ufaransa baada ya safari za ndege kutoka na kuingia mji mkuu Port-au-Prince kukatizwa kutokana na vurugu za kisiasa nchini Haiti. Paris imesema kuwa wizara ya ulinzi ndio itakayoshughulikia safari hizo, ambazo zilitarajiwa kuanza Jumapili.

Wizara hiyo imesema katika taarifa kuwa ubalozi wa Ufaransa mjini Port-au-Prince utasalia wazi na bado unaendelea na shughuli zake licha ya mazingira magumu.

Wafanyakazi wa ubalozi huo wanashirikiana kwa karibu kutoa msaada kwa jamii ya Wafaransa walioko nchini humo. Wizara hiyo imeongeza kusema kuwa karibu raia 1,100 wa Ufaransa wanaishi Haiti, wengi wao wakiwa na uraia pacha. 

Zaidi ya watu 33,000 wamekimbia mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince mwezi huu wakati mji huo ulipotekwa na magenge yenye silaha na kusababisha machafuko ya kisiasa katika taifa hilo.