1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel: Kitisho cha kutopewa silaha cha Biden kinasononesha

Sudi Mnette
9 Mei 2024

Balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa,Gilad Erdan ameelezea kusikitishwa na kitisho cha Rais wa Marekani Joe Biden cha kusitisha baadhi ya silaha kwa Israel iwapo itavamia mji wa Rafah uliofurika watu wengi wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4ffRq
Balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa,Gilad Erdan.
Balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa,Gilad Erdan. Picha: John Angelillo/UPI Photo/Newscom/picture alliance

Akizungumza na radio ya umma ya Isreal, Erdan ameiita kauli hiyo kuwa ni ngumu na ya kukatisha tamaa sana kusikika kutoka kwa rais ambaye amekuwa upande wao tangu mwanzo wa vita. Hiyo ni kauli ya kwanza tangu kutolewa kwa onyo la Rais Biden.

Soma pia:WHO: Hospitali za Rafah kukosa mafuta ndani ya siku tatu


Israel imekaidi mapingamizi ya kimataifa kwa kupeleka vifaru na kufanya katika mji huo wa mpakani, ambao inasema ni nyumbani kwa vikosi vya mwisho vya Hamas lakini pia umejaa watu wa Palestina waliokimbia makazi yao.

Awali akizungumza na kituo cha televisheni cha CNN, Rais Biden alisikika akisema kama Isreal itaingia Rafah, hatotoa silaha zitakazotumika, likiwa onyo lake kali la mwanzo tangu kuanza kwa vita hivyo.