Masuala ya Jamii
Umeme warejea visiwani Zanzibar
Baada ya Kisiwa cha Zanzibar huko Tanzania kubakia kutokuwa na
umeme kwa karibu miezi mitatu, jana jioni umeme ulirejea, lakini sio
katika sehemu zote za kisiwa hicho.
Kuna sehemu kadhaa hadi sasa
hazina umeme. Ukosefu wa umeme Kisiwani humo uliziathiri shughuli
za kibiashara, hasa za utalii katika kisiwa hicho, wacha tena za
kijamaa. Thelma Mwadzaya alizungumza na mwandishi wetu, Salma Said huko
Unguja mjini, na kumuuliza vipi Wazanzibari wamepokea habari za
kurejea umeme....
Mtayarishaji: Thelma Mwadzaya
Mhariri: Othman Miraji