Mashindano ya kandanda ya Kombe la Mataifa ya Afrika sasa yameingia nusu fainali baada ya michuano ya robo fainali ya mwisho wa wiki, huku waandalizi wa mashindao hayo, Gabon na Guinea ya Ikweta, zikiyaaga.
Kutakuwa na mechi mbili nchini Guinea ya Ikweta ambapo Zambia na Sudan wataumiza nyasi katika mji wa Bata na kisha mchuano baina ya wenyeji Guinea ya Ikweta na Cote d'Ivoire mjini Malabo katika robo fainali. (05.02.2012)
Kutakuwa na mechi mbili nchini Guinea ya Ikweta ambapo Zambia na Sudan wataumiza nyasi katika mji wa Bata na kisha mchuano baina ya wenyeji Guinea ya Ikweta na Cote d'Ivoire mjini Malabo katika robo fainali.
Emmanuel Badu ameikatia Ghana tiketi ya mechi za robo fainali katika dimba la Mmataifa ya Afrika baada ya kufunga bao lililowasaidia kutoka sare ya goli moja dhidi ya Guinea hapo jana.
Bao lake mchezaji Pierre Emerick Aubameyanga ambalo liliipa ushindi Gabon dhidi ya Tunisia mjini Franceville hapo jana liliwapeleka wenyeji hao wa kombe la mataifa ya bara Afrika hadi kileleni mwa kundi C.
Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.de.
Pata huduma zetu kupitia za SMS, RSS, Kijarida na huduma nyengine za mtandaoni kutoka DW.