Nchini Burundi Faustin Ndikumana mwanaharakati wa shirika linaloagiza wananchi kubadili mwenendo katika kukabiliana na maswala tete, kama rushwa, amefungwa jela.
Hali ya usalama inaripotiwa kuwa nzuri katika eneo la Moyale kaskazini mashariki mwa Kenya.
Vikosi vya Syria hii leo (08.02.2012) vimeyashambulia maeneo ya mkoa wa Homs kwa siku ya tano mfululizo, na kuwauwa karibu watu 47. Eneo hilo ni kitovu cha maandamano ya kuupinga utawala wa Assad.
Majeshi ya Syria yameuzingira mji wa Homs na kufanya mashambulizi makubwa wakati huu ambapo Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, akiwasili nchini humo kwa ajili ya mazungumzo na Rais Bashar al-Assad.
Rais wa visiwa vya Maldives, Mohamed Nasheed, amejiuzulu hii leo (07.02.2012) baada ya vikosi vya polisi kuanzisha uasi kufuatia wiki tatu za maandamano ya upinzani unaodai kuachiwa huru rais wa mahakama ya jinai.
Baada ya miaka mingi ya mivutano na uhasama baina ya kundi la Hamas na chama cha Fatah ndani ya Palestina, hatimae makundi hayo yamefikia maridhiano ya kuwa na serikali ya mpito ya Umoja wa Kitaifa.
Vikosi vya serikali nchini Syria vimeushambulia mji wa Homs hii leo (06.02.2012), na kuwauwa watu 50 katika mashambulizi yanayoendelea katika wilaya kadhaa za mji huo. Nazo Urusi na China zimetetea kura zao za turufu.
Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa
Tembelea DW katika Facebook
Tembelea DW katika Twitter
Pata huduma zetu kupitia za SMS, RSS, Kijarida na huduma nyengine za mtandaoni kutoka DW.